A unique combination of education, trans-cultural research and worldwide network

2017 Mafunzo ya kwanza ya Kampasi ya Muziki ya Afrika Mashariki – Addis Ababa

Septemba 08-30 2017
Mafunzo ya kwanza ya Kampasi ya Muziki ya Afrika Mashariki 

Mafunzo ya siku 23 kwa ajili ya wafanyakazi vijana kutoka taasisi 6 washirika (Ethiopia, Kenya, Sudan Kusini, Sierra Leone, Tanzania na Uganda). Kila nchi mshirika atapeleka kikundi cha wafanyakazi vijana hadi 7 katika mafunzo ya kina katika muziki.

Siku 23 za mafunzo ya muziki kwa wafanyakazi kutoka katika taasisi 6 zitafanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Kampasi hiyo inaratibiwa na kuenedshwa na GMA Berlin kwa kushirikiana na Jazz Amba Music School na Goethe-Institut nchini Ethiopia.

Programu hii itaanza na awamu tatu za mafunzo ya kina kwa viongozi vijana juu ya namna ya kutumia mtaalamu mpya wa miaka miwili uliotengenezwa kwaajili ya Afrika Mashariki. Siku nne za mwisho za mafunzo hayo zitalenga katika kutengeneza mtaala ambapo wakongwe katika utamaduni wataalikwa kushiriki, kuandaa mtaala mpya, na kuwaonyesha kwa vitendo washiriki wa mafunzo namna ya kuutumia mtaala huo wakati siku ya mwisho ya programu imetengwa kwaajili ya washiriki wote kufanya onyesho.

Vipengele vitakavyofundishwa katika wasrha hiyo ni pamoja Body Percussion, kusoma na kuandika nota, kusoma melodi, Harmony na Mafunzo ya kusikia/Sikio, Harmony ya kinanda, kunukuu, Mafunzo, kucheza ala na ubunifu. Kuna wakufunzi 6 wenye uzoefu, watatu kutoka Berlin, wawili kutoka Ethiopia na mmoja kutoka Zimbabwe. Mitaala hii inatoa mfumo kwa ajili ya mpango wa miaka miwili katika weledi wa mafunzo ya muziki.

Mtaala umetengenezwa maalum kwa ajili ya matumizi katika shule za muziki katika eneo hilo na kuruhusu mashirika ya washirika kutoa taaluma yenye weledi katika mafunzo ya muziki kwa kutumia European Credit Transfer System (ECTS) kwa kutumia Matokeo ya Kujifunza, Modules, Module maelezo na Points mikopo. mpango unalenga katika kutumia ujuzi na ubunifu katika mtaala wa muziki – kusoma na kuandika muziki wa Afrika na pia kutumia mbinu za kina za kubuni mapigo na kuchanganya ladha mbalimbali za muziki (Music Ensemble), pia kutumia video kama nyenzo ya kufundishia.

Mtaala unaenda sambamba na upewaji wa leseni ili wanafunzi wanaosoma waweze kupata kutambuliwa na kutunukiwa vyeti kupitia Vyuo vya elimu ya ufundi katika nchi zao (TVET). Wanafunzi watajifunza jinsi ya kunukuu muziki kutoka nchi zao na kutumia nukuu hizo katika kukuza mitaala na kuongeza maudhui yake kulingana na mahitaji yao. Uandishi na uhifadhi huo wa muziki utatumika pia kutengenezea mbinu mpya za kufundishia ambapo wanafunzi pia watajifunza namna ya kutengeneza mtaala ikiwa ni njia moja wapo ya kujifunza.