A unique combination of education, trans-cultural research and worldwide network

2017 Mkutano wa kwanza wa Mradi Kampala

26 – 27 Aprili 2017
Mkutano wa kwanza wa Mradi

Huu ni mkutano wa siku mbili ambao umewakutanisha washirika wetu na kuratibiwa na  wenyeji wetu Bayimba Cultural Foundation katika kituo cha Goethe-Intitut mjini Kampala nchini Uganda mwezi Aprili 2017.

Wawakilishi walioteuliwa na washirika wetu kutoka katika kila nchi wanakutana kuhitimisha uaandaji wa mbinu za ufundishaji, ratiba, na maudhui ya shughuli nzima za mradi ikiwa ni pamoja na kuamua malengo na majukumu ya kila mshiriki katika kutekeleza mradi, kuripoti, mambo ya vifaa na usambazaji. Mkutano unamalizika kwa kutiwa saini kwa Mkataba wa Makubaliano kati ya washirika.