A unique combination of education, trans-cultural research and worldwide network

2017 Warsha ya kwanza ya kujengea uwezo mashirika – Kampala

Aprili 28 – Mei 7 2017
Warsha ya kwanza ya kujengea uwezo mashirika

Warsha kubwa ya kwanza inalenga kuendeleza uwezo wa mashirika washirka wa kuunganisha programu za mafunzo kwa vijana katika sanaa katika shughuli zao katika nchi zao husika.

Warsha hiyo ya siku 9 itajumuisha mafunzo ya IT, usimamizi wa maudhui, kusimamia mawasiliano ya jamii, utawala katika shule za muziki, kibali, kuanzisha na kuendesha biashara endelevu ya kijamii.

Wafanyakazi wawili wenye wajibu wa usimamizi wa miradi katika kila nchi washirika watahudhuria mafunzo ambayo yatafanyika sambamba na Soko la Muziki Afrika Mashariki (DOADOA) Uganda (3 – 6. May 2017). Hii itawezesha washiriki kuendeleza nguvu ya ushirikiano na mtandao kwa ajili ya kubadilishana mbinu bora na kuendeleza mawazo ya mradi kitaifa na kikanda.

Katika warsha ya kwanza washiriki watajifunza jinsi ya kutengeneza muundo wa mashirika yao kwa kuzingatia mahitaji ya kiufundi na vigezo vya kisheria kutoka katika nchi zao (Miongozo, kanuni za masomo, kanuni za mitihani, mahitaji ya kujiunga, taratibu za kuchagua) kwa kutumia mifano iliyoandaliwa tayari. Kutumia mfumo huu, wataweza kutengeneza na kujifunza jinsi ya kutumia mfumo jumuishi wa usimamizi wa ofisi ambao utazingatia mahitaji ya kupewa leseni chini ya mfumo wa TVET katika kila nchi.

Washirika pia watafanya utafiti na kutengeneza mahitaji ya mfumo kwa ajili ya kutengenezea mfumo maalumu wa kompyuta unaotumika kuandaa programu kwaajili ya mafunzo yasiyo rasmi katika utawala wa muziki (Computer Based Enterprise Resource Planning Program) uliundwa kwa ajili ya matumizi katika mafunzo vijana.

Aidha, warsha itajumuisha mafunzo ya kuwajengea uwezo binafsi kwa mameneja wa mradi. Hii ni pamoja na kubadilishana mbinu bora, mafunzo katika utayarishaji wa mradi, ukusanyaji wa fedha, masoko na kujenga mawazo ya ushirikiano wa kikanda.

Kwa sababu ya ukaribu na Soko la Muziki Afrika Mashariki (DOADOA) washiriki watatakiwa kuwasilisha mawazo ya mradi walioandaa wakati wa mafunzo ili kuruhusu washiriki kupata uzoefu wa kutangaza mawazo yao ya miradi kwa watu wengine. DOADOA ni jukwaa la kipekee linaloleta pamoja wataalamu katika sekta ya muziki Afrika Mashariki (mameneja, sekta ya elimu muziki, masoko, waandaaji wa matamasha, kampuni za kurekodi nk). Hii itawawezesha kujenga mawazo mapya, kupanua nafasi zao kimtandao, kupata ufahamu katika fursa mpya katika viwanda na kutengenza miradi ya kikanda ili kusambaza matokeo ya mradi katika eneo hilo.