A unique combination of education, trans-cultural research and worldwide network

2018 Kampasi ya pili ya muziki ya Afrika Mashariki – Addis Ababa

Septemba 11 – Oktoba 4 2018
Kampasi ya pili ya muziki ya Afrika Mashariki

Hizi ni siku 23 kwa ajili ya wafanyakazi vijana kutoka taasisi 6 washirika (Ethiopia, Kenya, Sudan Kusini, Sierra Leone, Tanzania na Uganda). Kila nchi mshirika itapeleka kikundi cha wafanyakazi vijana hadi 7 katika mafunzo hayo ya kina ya muziki.

Mafunzo hayo ya siku 23 yatafanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Kampasi itaratibiwa na kuendeshwa na GMA Berlin kwa kushirikiana na Jazz Amba Music School na Goethe-Institut nchini Ethiopia.

Programu italenga katika mtaala bunifu wa miaka 2 ambao utakuwa umetengenezwa kwaajili ya kanda. Kutakuwa na awamu tatu za mafunzo ya siku nne. Siku nne za mwisho zitatengwa kwaajili ya kutengeneza mtaala ambapo washiriki wataangalia mbinu za kina za kurekodi na kunakili muziki. Siku ya mwisho itatengwa kwaajili ya washiriki kufanya onyesho la muziki.

Mada zitakazofundishwa ni pamoja na Mnyumbuliko wa mwili (Body Percussion II), Kusoma na kuandika Rythm II, melodic Reading II, Harmony & Mafunzo ya Sikio II, Harmony ya Kinanda II, mafunzo ya kunakili, Ala na Ensemble. Kuna wakufunzi wenye uzoefu 6, watatu kutoka Berlin, wawili kutoka Ethiopia na mmoja kutoka Zimbabwe. Mitaala hii inatoa mfumo wa programu ya miaka miwili katika mafunzo ya kiweledi katika muziki.