A unique combination of education, trans-cultural research and worldwide network

2018 Warsha ya kujengea uwezo taasisi  – Kampala

Mei 03-12 2018
Warsha ya kujengea uwezo taasisi

Warsha ya pili itafanyika ili kuwajengea uwezo washirika ili kuweza kuingiza mafunzo hayo katika shughuli zao za sanaa katika nchi zao.

Sehemu ya pili ya warsha ya siku 9 itajumuisha mafunzo ya kina katika IT, kozi zaidi juu ya usimamizi wa maudhui, kusimamia matumizi ya mitandano ya kijamii, utawala katika shule za muziki, vibali na usimamizi wa fedha ya biashara endelevu ya kijamii. Mada za uandishi wa miradi kutokana na matokeo ya utafiti uliofanywa kwa washiriki katika semina 2017 utaruhusu washiriki kupata utambuzi wa mchakato wa kuandika miradi ya kuomba ruzuku kwa kuandika maombi yao ya ruzuku.

Washiriki kujifunza mbinu ya tathmini na jinsi ya kuandaa takwimu zilizokusanywa kutoka utafiti na madodoso kwa ajili ya kuyatumia katika kuwasilisha ripoti. Baada ya kuwa wamejifunza mambo ya vibali na leseni katika semina ya kwanza, wataanza kutumia ujuzi huo katika kushawishi na kuweka makubaliano na mamlaka husika za utoaji vibali na leseni katika nchi zao.

Kulingana na matokeo ya utafiti na utafiti katika kampasi ya kwanza rasimu ya kielelezo cha mahitaji ya mfumo wa kompyuta (Computer Based Enterprise Resource Planning Program Based Enterprise) utawasilishwa, kujadiliwa na kukamilishwa.

Washirika pia wataendeleza mawazo ya miradi ya kitaifa na kikanda wakati wa kipindi cha kujadiliana, kuendeleza na kuboresha mikakati ya usambazaji wa shughuli zao. Soko la Muziki Afrika Mashariki (DOADOA), ambalo huendeshwa kwa wakati mmoja na semina hii, litawaruhusu kuwasilisha mikakati yao ya usambazaji wa kazi zao na kupanua nafasi zao kimtandao, kupata ufahamu wa mwenendo mpya katika sekta ya muziki na kuendeleza miradi kikanda na kusambaza matokeo ya mradi katika eneo hilo.